
National Arts Council BASATA
09/09/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba,
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam, Tanzania. Telephone: 2863748/2860485, Fax: 0255 – (022) – 286 0486 E-mail: basata06@yahoo.com, Mob: +255 715 825 059, +255 752 475 941
WADAU WA SANAA NA WAMILIKI WA KUMBI
WATAKIWA KUSAJILI NA KUPEWA VIBALI
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) amewataka wasanii na wadau wote wanaojihusisha na
shughuli za Sanaa kuhakikisha wanakuwa na usajili wa BASATA na kupewa vibali
vya kuendesha shughuli zao.
Wadau wanaopaswa kujisajili na
kuhakikisha wanakuwa na vibali vya kuendesha shughuli za Sanaa ni pamoja na
wasanii binafsi, vikundi vya wasanii,Bendi za muziki, wakuzaji Sanaa maarufu
kama Mapromota/m
ameneja, studio za kurekodi muziki na
wamiliki wa kumbi zinazotumika kwa ajili ya maonesho ya shughuli za Sanaa zikiwemo
disko, harusi na sherehe mbalimbali zenye kupambwa na sanaa ama burudani.
Zoezi hili la usajili na utoaji vibali
ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuirasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwatambua
wadau wote wanaojishughulisha na kazi za Sanaa ili waweze kufanya kazi kwa kufuata
misingi ya sheria, kanuni, maadili na taratibu zilizowekwa na kuepuka uholela jambo
ambalo ni moja ya chanzo cha wizi wa kazi za wasanii, mmomomyoko wa maadili udanganyifu
katika mikataba ya kazi za Sanaa na changamoto nyingine zinazotokana na
shughuli za Sanaa na kupelekea ugumu kwa Serikali wakati wa kutatua changamoto
hizo
Kaimu Katibu Mtendaji amefafanua kwamba
kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 ni kosa Kisheria kwa wadau
wa Sanaa kuendesha shughuli zao bila kusajiliwa na kupata kibali toka BASATA.
Aidha, anasisitiza kwamba ili kuepuka
usumbufu ni vema wadau wote ambao hawajasajiliwa na wale ambao hawajahuisha
vibali vyao kuhakikisha wanafanya hivyo mapema iwezekanavyo ili kuepuka
usumbufu usio wa lazima.
Sanaa
Ni Kazi, Tuikuze Na Kuithamini
Godfrey
Mngereza
Katibu Mtendaji(K)






0 Comments:
Post a Comment