BENDI ya muziki wa taarabu ya Jahazi, inatarajia kufanya onyesha bab kubwa katika Ukumbi wa Travertine, Julai 3 mwaka huu, katika kusherehekea Sikukuu ya Iddi.
Mratibu wa onyesho hilo kuoitia Kampuni ya Cash Money, Abbas Chanztemba, alisema onyesho hilo litakuwa la kwanza katika ukumbi huo wa Travertine, baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani unaoendelea sasa.

Pamoja na burudani hiyo kutoka kwa Jahazi, pia zawadi mbalimbali zitatolewa kwa mashabiki watakaohudhuria onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la aina yake.
“Hili litakuwa onyesho la kwanza kufanyika katika ukumbi wa Travertine baada ya mfungo, hivyo kutakuwa na zawadi kibao, mojawapo ikiwa ni ubuyu, tende na halua, ambazo atapewa kila shabiki atakayepita mlangoni,” alisema Chanztemba.

0 Comments:
Post a Comment