National Arts Council BASATA
Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza
la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za misiba ya wasanii
watatu wa tasnia ya filamu na muziki nchini.
“
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya vifo hivi vya
wasanii hawa John Mganga, Mlopelo na Hussein Mkeity a.k.a Sharo Milionea ambao
mchango wao unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo waliloliacha ni
kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa
pole kwa familia za marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa
subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na wapendwa wetu.
Tunaomba
mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu. Baraza liko
pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,
tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.
Imetolewa
na
Ghonche
materego
Katibu
Mtendaji
Baraza
la Sanaa la taifa.
0 Comments:
Post a Comment