Kutokana
na kushuhudiwa kwa mmomoyoko wa maadili katika sekta ya sanaa katika
siku za hivi karibuni, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limeandaa
kongamano la pamoja la wadau kujadili juu ya hali hiyo ili kupata
mapendekezo ya nini kifanyike na hatua gani zichukuliwe kukabiliana na
hali hiyo.
Katibu
Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, amesema kongamano hilo
litafanyika Jumatatu ya terehe 15/10/2012 katika Jukwaa la Sanaa kuanzia
saa 4:30 asubuhi ambapo mada itakuwa ni ‘Mchango wa vyombo vya habari
katika kudhibiti au kuchochea mmomonyoko wa maadili katika sekta ya
sanaa’.
Ghonche
amewakaribisha wadau wote ili kuleta michango, mapendekezo na hoja
mbalimbali katika kuleta mustakabali utakaojenga sekta ya sanaa yenye
maadili na itakayokuwa na tija kwa utamaduni wa taifa.
Amesema
kongamano hilo litaongozwa na Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari
na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) Dkt.
Herbet Makoye ambaye atakuwa Mwenyekiti, na wajumbe wazungumzaji
watakuwa ni Bishop Hiluka (mwandishi na mtunzi), Harrieth Makweta
(mwandishi) Khadija Khalili (mwandishi), Wilson Makubi (Katibu
Shirikisho la Filamu) Ado Novemba ambaye ni Rais wa Shirikisho la
Muziki, Edna Rajabu (TBC).
Hatua
hiyo ya BASATA imekuja wiki moja baada ya kutoa maelekezo kwa
mashirikisho ya sanaa kushughulikia suala la mmomonyoko wa maadili na
kuwachukulia hatua wasanii wanaohusika na vitendo vya kujidhalilisha na
kuidhalilisha tasnia ya sanaa na jamii kwa kuwa nusu utupu au kuandaa
sanaa zinazokiuka maadili.
0 Comments:
Post a Comment