WATU saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kituo cha Mbagala Kizuiyani baada ya kukamatwa na Polisi wa kituo hicho wakiwa na kazi feki za wasanii zenye thamani ya Sh11 milioni.
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni maalum ambayo inaendeshwa na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Kampuni ya Msama Action Mart.
Mbali na CD na Dvd feki ambazo zimekamatwa pia wamekamata mitambo miwili ambayo inatumika kudurufu kazi hizo ambazo pia kulikuwa na stika mpya za kung'aa za Kampuni ya Stemps ambazo zinatumika kwenye filamu mbali mbali za wasanii wa bongo.
CD na Dvd feki nyingi zilizokamatwa ni za wasanii Rose Muhando, Bahati Bukuku, Solomon Mukubwa, Vicent Kigosi 'Ray' JB na zile za vichekesho za msanii King Majuto pamoja na albam ya Aleluya Collection.
Akizungumza katika operesheni hiyo Mkurungenzi wa Msama Promosheni, Alex Msama alisema "Inasikitisha kwa kweli huu wizi wa kazi za wasanii umeota mizizi, watu wanamitambo ya kisasa kabisa yenye uwezo wa kudurufu nyimbo 6,000 mpaka 10,000 kwa saa.
"Kibaya zaidi mpaka ndugu wa vigogo wabunge na Polisi wanahusika, tena bila aibu kama Dodoma vigogo wanakuja kabisa wanakwambia tuwaachie ndugu zao, tutawaweka wazi siku si nyingi."alisema Msama.
Watu hao saba wamekamatwa ikiwa ni siku moja baada ya wasanii wote wa bongo fleva, filamu na bendi kuungana na kutoa tamko la pamoja kwa kutaka serikali iharakishe sheria mpya ya kuwadhibiti maharamia wa kazi zao kabla hawajajichukulia hatua mikononi mwao na Jumatano ijayo wameandaa matembezi ya amani kupinga uharamia wa kazi za wasanii ambayo yataanzia kwenye viwanja vya Leaders Clab.
Naye Askari wa Upelelezi kituo cha Kizuiyani Khalid Abubakar alisema "Jumatatu watuhumiwa wote watapelekwa mahakamani pale Temeke ili sheria iweze kuchukua nafasi yake, tumekuwa tunalalamikiwa watuhumiwa wanakamatwa lakini wakifikishwa mahakamani wanalipa faini wanatoka, lile ni suala la mahakama sisi hatuna amri nayo cha msingi ni sheria ibadilishwe kwa kuongezewa makali.
"Ugumu upo kwa wanaodurufu wanawapa machinga na ndio wamekuwa wakikamatwa sana wakati wahusika wakuu wanaudurufu tunashindwa kuwapata, na hata wakipatikana sheria haiwabani kwani wanalipa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miaka mitano sasa wengi wanakuwa na uwezo wa kulipa faini na kutoka.
Hata hivyo tayari serikali imeweka wazi kuwa kuanzia Januari sherial mpya ya kudhibiti kazi za wasanii itaanza kutumika ikiwa ni pamoja na kuweka stika za Mamlaka ya Mapato |Tanzania (TRA), kudhibiti kazi hizo.
Saturday, August 11, 2012
saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi na kazi feki za wasanii zenye thamani ya Sh11 milioni.
Saturday, August 11, 2012
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 Comments:
Post a Comment