Monday, November 28, 2011

Tamasha la Str8t Music lafanya vizuri Dar

Wataalamu wa mambo ya Burudani nchini Str8Muzik Festival Inter-College Special 2011 la vyuo la mwaka 2011 lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam, Jumamosi na kuhudhuriwa na maelfu ya watu, limefana na kupambwa na mkali wa Hip Hop toka Marekani, Fabulous aliyewarusha vijana wa kike na kiume.

Baada ya hapo wasanii toka Bongo walipagawisha wapenzi hao walifurahia na kuimba pamoja na kundi hilo lenye vijana watatu wakati huo, Inspekta Haroun naye aliibuka na kufanya vitu vyake wakati huo, Amani Temba 'Mheshimiwa Temba' na Chege nao walikamua kwa ngoma zao.

Elius Barnaba na sauti yake tamu alikuja akiwa na kundi lake la THT kufanya makamuzi yao, walicheza na kuaacha mashabiki wakifurahia huku Mfalme wa Rhyme, Afande Sele akipata wasaa wake wa kupiga shoo.Pina wa Kikosi cha Mizinga alikamua na ngoma yake ya Umoja ni Nguvu na kuungwa mkono na wapenzi wa muziki waliokuwa wanamshangilia na kudhihirisha kuwa rapu si tu kwa Fabolous, bali hata kwa Wabongo.
Wana-Hip Hop kutoka Arusha Nako 2 Nako waliruka stejini na baadaye kupigwa tafu na wakali Jo Makini na Niki wa Pili.Usiku huo ulipambwa pia na MwanaFa na Shetta waliofanya vitu vyao na kufuatiwa na Diamond Platinum kabla ya Big Boy Baghad aliyefuatiwa na Juma Nature kutoka Wananume Halisi.Wateule nao hawakuwa nyuma wakati Mchizi Mox na Jay Mo walikamua na kuwapagawisha wapenzi na sauti zao.Kwa kumalizia shoo hiyo, Fbolous alikamua ambapo kabla ya hapo alitoa salamu maarufu kwa vijana wa Bongo ya 'mambo vipi' iliyowapagawaisha watu zaidi.
Mkali huyo akiwa amevalia koti la jinsi lenye rangi ya bluu na shati jeusi alikamua nyimbo 20 na kudhihirisha kuwa zilikuwa ni saa zilizosubiriwa kwa hamu sana wapenzi hao kwa saa tisa.
Tamasha la StrMuzik lilianzishwa mwaka 2005 na baadaye lilijilikana kama Inter-College Bash, lilifanyika Dar es Salaam na mwaka 2008 lilifika hadi Mwanza, Morogoro na Dodoma.

0 Comments: