Monday, November 28, 2011

Mr II aitikisa Dar katika uzinduzi wa albamu ya ANTiVIRUS...

MKALI wa muziki wa Hiphop nchini, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu jumamosi alitikisa jiji la Dar es Salaam baada ya kutoa burudani kali wakati wa uzinduzi wa albamu yake iitwayo Anti Virus.

Sugu ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini juzi alionyesha kuwa bado ni mwamba katika fani hiyo baada ya kutoa burudani kwa kuimba nyimbo zake za zamani zilizoamsha maelfu ya vijana na wazee waliohudhuria uzinduzi huo.

Uzinduzi wa albamu hiyo ulifanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii kusindikizwa na wasanii wengine wengi akiwemo Adili na Soggy Doggy Hunter. Sugu ambaye alipanda jukwani saa sita usiku, alisababisha mashabiki kupiga kelele huyu yeye akiwahoji mashabikia hao kile wanachokitaka.
"Oyoooo, Oyoooo nawashukuruni sana kwa kutuunga mkono leo ninaweka uheshimiwa pembeni na kushusha mawe, pigeni kelele mpaka walioko Leaders wasikie,"alisema Sugu.

Baada ya hapo akaanza na wimbo wake uitwao 'Sugu Moto Chini' ambao uliwaamsha mashabiki kwa furaha na baada ya hapo akachombeza mashairi kadhaa ya wimbo ulitwao 'Yamenikuta' na kisha kupiga wimbo mwingine uitwao 'Kiburi' aliomshirikisha Stara Thomas.

Hakuishia hapo, akaimba wimbo mwingine uitwao 'Mambo ya Fedha' ambapo kabla kuanza kuimba baaddhi ya wabunge wa Chadema kama John Mnyika(Ubungo), Joyce Mukya na Regia Mtema(Viti Maalum-Chadema), Highness Samson(Ilemela) walipanda jukwaani na kucheza pamoja na Sugu wimbo huo.
Sugu aliendelea kuporomosha nyimbo zake nyingine kama 'hayakuwa mapenzi' na mwisho akaimba wimbo wenye jina la 'Sugu' ambao ulishangiliwa kwa kelele nyingi.

Kabla ya kushuka jukwaani Sugu alisema yuko mbioni kufanya wimbo na kumshirikisha mheshimiwa mmoja ambapo alimpandisha jukwaani mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe alipopanda jukwaani akanza kwa mbwembwe za kuwasalimia mashabiki kwa kusema, 'Oyoooo Oyoooo nafurahi mnacheza na kwa ruhusa ya watu wa usalama naomba Sugu na wenzake waimbe kwa dakika 10 tena."

Katika uzinduzi huo Sugu alisindikizwa na wasanii kama Danny Msimamo, Mabaga Fresh walioonyesha kwamba bado wamo, Mgosi Mkoloni, Mapacha, Suma G.

0 Comments: