Tuesday, July 19, 2011

TUZO ZANGU ZITADUMU MILELE-KING KIKI

KING KIKI
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Kikumbi Mwanza Mpango "King Kiki"amesema tungo zake zitadumu milele katika hazina na tungo za muziki huo kutokana na jinsi jamii inavyozipokea.

King Kiki alisema kwamba tungo zake ambazo alizitunga zamani akiwa na bendi tofauti,zinaonekana kupendwa na washabiki wake wengi na hali hiyo inajitokeza pindi akiwa na bendi yake ya sasa,Yacapitale Bara Moto"Wazee Sugu" ambapo washabiki wake hufika kwa wingi na kuomba tungo hizo.

"Tungo zangu zitapendwa milele,hata mungu akinichukua ninahakika nitakuwa nimeacha uridhi kwa washabiki wake ambao wengi wake wameonyesha kugushwa na tungo hizo na huwa nifarijika sana na hali hii,hakika hata mungu akija kunichukua,nitakuwa nimeacha uridhi ambao jamii nzima inaupenda" alisema.

Alisema kwa sasa,bendi yake imeongeza umahiri katika utendaji wake kutokana na vyombo hivyo,ambavyo vimeboresha hata sauti za tungo zake.
"Baada ya kuongeza vyombo kwa sasa,tunafanya kazi kwa nguvu zote,kuhakisha tunawapa washabiki kazi nzuri" alisema.

Pamoja na kutamba na vibao vyake kadhaa,vibao ambavyo vimeonekana kumpa umaarufu mkubwa ni Zibola(kitamba cheupe),Kasongo urudie,Mimi Chuma, Mimi Msafiri,safari ya London na vingine kadhaa.

Na James Nindi

0 Comments: