Friday, July 29, 2011

Mwanamuziki Ludacriss awasili nchini TANZANIA


Msanii na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani Christopher Brian Bridgers a.k.a Ludacriss jana nchini kwa ajili ya kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2011 litakalofanyika kesho katika uwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mwanahip hop huyo ambaye aliwasili saa nane mchana, alishindwa kutoka nje ya uwanja huo kwa muda wa saa zima akikwepa kunaswa na kamera za waandishi wa habari na hakutaka kabisa kuzungumza chochote.

Mkurugenzi wa Maendeleo wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba alisema
shamra shamra za kufikia kilele cha miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011 zitakuwa tofauti na zenye msisimko mkubwa ikilinganishwa na miaka mingine yote iliyowahi kufanyika.

“Kesho ndio kilele cha tamasha hili hivyo tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na msisimko mkubwa ukilinganisha na hapo nyuma, kwani tamasha hili ni kubwa katika anga ya burudani ndani na nje ya Tanzania"alisema Ruge.

Stori na Mdau wetu

0 Comments: