Wednesday, July 20, 2011

MH RAIS KIKWETE AMWAMBIE MH NCHIMBI ALISHUGHULIKIE SUALA LA WIZI WA KAZI ZETU-RAS LION

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Gerald Simba a.k.a Ras Lion amemwomba Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete kuwasaidia wasanii kwa kumwagiza waziri wa Utamdauni,michezo na Habari,Dk Emanuel Nchimbi kujituma zaidi katika utendaji wake ili kudhitibi wizi wa kazi za wasanii ili waweze kufaidika na malipo ya kazi zao.

Msanii huyo alisema kwa nia ya wasanii wenzake anafikisha kilio bhicho kwa Mhe Rais Jakaya Kikwete kutokana na suala ya wizi kuzidi kukua kila kukicha hapa nchini huku Serikali ikisema ipo sambamba na wasanii katika kudhibiti suala la wizi wa kazi zao ila tatizo hilo linazidi kukua siku hadi siku ambapo kwa siku za karibuni,wizi hao wanafanya kazi zao bila kificho.

"Namuomba Rais amkumbushe tena waziri wetu,Dk Nchimbi,siku hizi wizi wa kazi zetu,wapo mitaani na tena wanafanyia kazi zao bila kificho na huku sheria ikiwepo serikali imetupa,tunaibiwa kazi zetu bila kificho na hakuna ambaye anatusaidia mpaka wasanii tunaelekea kuacha muziki sasa na kujikita katika shughuli nyingine za kujiingizia kipato,"alisema.

Msanii huyo alidai hata taasisi iliyoundwa na Serikali*COSOTA" kwa nia ya kuwasaidia wasanii kulinda kazi zao inaonyesha kushindwa kazio hiyo kutokana na ukubwa wa tatizo hilo,kuzidi kukua kila kukicha.

Na James Nindi

0 Comments: