Monday, July 4, 2011

Black Rhyino kuajichia ngoma mpya ya Taking Over hivi karibuni

Black Rhyino
MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nicaulaus Haule a.k.a Black Rhyino amesema yupo mbio kurekodi video ya kibao chake kipya Taking Over katika siku za karibuni.

Black Rhyino alisema baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu,akipima upepo wa muziki huo,umefikia wakati kwake kuanza kutambulisha kazi zake mpya na anatarajia kuanza kuitangaza video yake hiyo kwa nia ya kuwaonyesha washabiki wake kwamba kimya chake kilikuwa cha msingi..

"Natarajia kuanza kuitambulisha video yangu hii,ambayo ninatarajia kuanza kuirekodi muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu kadhaa ikiwa ni pamoja na kuiteua kampuni nitakayofanya nayo kazi hii"alisema.

Black Rhyino alisema kibao chake hicho kimerekodiwa na mtayarishaji mpya anayefahamika kwa jina la Mbezi,a.k.a The God Father ambaye bado hajawika sana katika fani hiyo lakini ana uwezo mkubwa na anachokifanya pia katika kibao chake hicho,amemshirikisha msanii Dogo Sabrano kwa nia ya kuongeza ladha ya kibao hicho.

Msanii huyu aliyewahi kutamba na vibao vyake kadhaa kikiwemo Mistari ambacho kilitokea kupendwa na washabiki wa muziki huo,kiasi cha kumpa sifa kemkem katika ulimwengu wa muziki.
Na James Nindi

0 Comments: