BENDI ya muziki wa dansi ya The B Band inayomilikiwa na msanii Banana Zorro imesema imeweka mikakati kadhaa kwa lengo la kujiweka imara kimuziki.
Mkurugenzi wa bendi hiyo,Banana Zorro alisema pamoja na bendi yake kuwa imara na kuwa na washabiki wengi,imezidi kujiweka imara kwa kuweka mambo mengine sawa.Kiongozi huyo alisema bendi yake imefikia baadhi ya maamuzi katika utendaji wake kwa nia ya kukabiliana na ushindani uliopo katika fani ya muziki nchini.
Banana alisema moja ya maazimio ambayo bendi yake imeyafikia ni pamoja na kuongeza kutoa tungo zake zilizo bora na kuzirekodi kwa nia ya kujitangaza kwa washabiki wake.
Katika kufikia hatua hiyo,kiongozi huyo alisema bendi yake imefikia maamuziki hayo kwa nia ya kujiweka imara zaidi kimuziki.Hata hivyo,Banana alisema bendi yake pia imeongeza vyombo vipya kwa nia ya kuifanya kutoa burudani iliyo bora zaidi.
"Haya ni mabadiliko ambayo bendi yetu,imeyafikia katika kuhakikisha tunafanya vizuri na kumudu ushindani ambao upo katika sekta ya muziki na sasa tumesharekodi albamu nzima,kwa kutumia studio tofauti za jijini Dar es Salaam zikiwemo Metro Records chini ya mtayarishaji Allan Mapigo,sambamba na studio nyingine pamoja na sasa tunamalizia kutengeneza video nne katika nyimbo hizo nazo zimesharekodiwa"alisema.
Na James Nindi
0 Comments:
Post a Comment