MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya Suma G amesema kimya chake cha muda mrefu kinakuja na mshindao mkubwa na hivyo washabiki wake wasubiri kuanza kusikia kazi zake mpya.
Akichonga na kona hii ya burudani,jijini Dar es Salaam jana,alisema kamba amekuwa kimya kwa muda mrefu,kutokana na sabau mbalimbali ikiwa ni paoja na kusoma mueekeao wa muziki ho toka kwa wasanii wapya.
Alisema mara baada ya kukamilisha harakati zake hizo,kwa sasa ameanza maandalizi ya kuanza kujitangaza upya kwa kuja na tungo zake mpya ambapo kwa sasa anaendelea na kazi ya kuzirekodi.
"Sipendi kuongea kwa sasa kwa kuwa sijakamilisha yale ambayo,ninayafanya,lakini napenda kuwajulisha washabiki wangu kwamba nipo na nakuja na kazi mpya,nilikuwa kimya nikisoma nyakati,sasa nipo kwa Maco Chali nafanya kazi na nitafanya na sehemu nyingine kuhakisha nakuja na kazi bora zaidi ya zile za mwanzoni" alisema.
Suma G,alisea uzoefu alionao katika fani hiyo,utampa nafasi ya kufanya kazi zilizo kuwa na kiwango cha juu,kutokana na uwezo mkubwa wa kisanii alionao katika muziki huo.
Aidha,akizungumzia hali ya muziki huo nchini kwa sasa,alisema muziki umebadilika katika sehemu mbalimbali,ikiwa ni pamoja na kuingia kwa wasanii wenye vipaji vikubwa kitu ambacho kimesaidia kuleta ushindani.
Suma G,msanii mwenye vituko vingi aliwahi kutamba na vibao vyake kadhaa vikiwemo Noma,Popote ikitokea na Vituko Uswahilini,amekuwa kimya kwa miaka kadhaa kujihusisha na masuala ya muziki.
Na James Nindi






0 Comments:
Post a Comment