Tuesday, June 28, 2011

PROFESA JAY ANAJIANDAA KUACHIA NGOMA MPYA

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule"Profesa Jay"amesema washabiki wake wategemee makubwa kwake kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu.


Profesa Jay alisema baada ya kuwa kimya kwa muda wa miaka kadhaa,kwa sasa anajiandaa kuja na kazi zake mpya na sasa ameshakamilisha tungo zake kadhaa,kwa nia ya kuanza kujitangaza baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa akiwa akijihususha na shughuli binafsi ikiwa ni pamoja na kufanya ziara nyingi za ulaya,Asia na Marekani.

"Albamu yangu ya sasa itakuwa na ubora wake kwa kuwa imeandaliwa katika sehemu mbalimbali hapa duniani,kutokana na kuwa na ziara nyingi za nje ya Tanzania"alisema.

Msanii huyo alisema kwa sasa anafanya kazi za mwisho ili kukamilisha kazi ya kurekodi tungo zilizobaki na kifanya albamu yake kutimia. Profesa Jay ni mmoja wasanii wenye washabiki wengi wa miziki huo kutokana na wengi wao kufurahishwa na utendaji wake kazi .

Na James Nindi

0 Comments: