Tuesday, June 28, 2011

MAUNDA ZORRO KUTAMBULISHA NYIMBO YAKE MPYA HIVI KARIBUNI

Maunda Zorro
MWANADADA na MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Maunda Zorro amesema hivi karibuni anatarajia kuanza kutambulisha kazi zake mpya mara baada ya kumaliza kipindi cha likizo ya uzazi.

Alisema kwa sasa anakaa na uongozi ambao unamsimamia katika kazi zake za kisanii ili kupanga ni nyimbo zipi aanze kuzutambulisha kwa washabiki wake. "Nilikuwa kimya kwa ajili ya likizo ya kujifungua,nashukuru mungu kwa sasa mtoto wangu ni mkubwa na ana umri wa mwaka mmoja sasa"alisema

Maunda alisema mtoto wake huyo ambaye ni wa kiume anayekwenda jina la Rishad kwa sasa amekuwa na hivyo kumpa nafasi ya kuweza kuwa na muda wa kuendelea na kazi zake za kisanii.
Alisema anahazina kubwa ya tungo ambazo alikuwa amezirekodi siku za nyuma ambazo hazijawahi kusikika kwa washabiki wake na hivyo anajipanga kuanza kuzitangaza.

Maunda alisema kuwa "Hata kama tunaibiwa,ila kwa sasa muziki unalipa siyo kama ambavyo walifanya wazee wetu zamani,mimi nawaomba wanamuziki na wasanii wenzangu nchini,tusikate tamaa kwa ajili ya wizi, badala yake tuzidi kufanya kazi tu" alisema.

Maunda Zorro ni dada wa mwanamuziki mahiri Banana Zorro wote wakiwa ni watoto wa gwiji wa muziki Zahiri Ally Zorro ambaye aliwahi kutamba na bendi mbalimbali za muziki katika miaka ya nyuma.
Na James Nindi

0 Comments: