MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Joseph Rushahu a.k.a Bwana Misosi amesema amefarijika sana na jamii jinsi ilivyoipokea kibao chake kipya cha Pilato wa Game ambacho amewashirikisha nyota wawili wa muziki huo nchini.
Akichonga na safuu hii ya Burudani jijini Dar es Salaam, alisema kwamba amefarijika sana na jinsi washabiki wake walivyokipokea kibao hicho kiasi cha kukifanya kuanza kupata mialiko ya kimuziki sehemu mbalimbali ikiwa ndani na nje ya nchi na kibao chake hicho ambacho amekitoa katika siku za karibuni kwa kuwashirikisha wasanii Fareed Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Juma Kassimu a.k.a Sir Juma Nature,kimejipatia umaarufu mkubwa katika anga za muziki kiasi cha kumpa mialiko kadhaa.
"Nawashuku sana washabiki zangu kwa njia walivyokipokea kibao changu hichi,hii imeonyesha mwangaza wa kufanya vizuri zaidi sababu mashabiki ndiyo walengwa,nawashukuru sana" alisema Bwana Misosi. Bwana Misosi alisema kibao chake hicho ni mwanzo wa utambulisho wa kazi zake kadhaa mpya ambazo zinatarajia kuzifanya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na majukumu ya kifamilia.
Msanii huyu ambaye alitamba na vibao vyake kadhaa vikiwemo,Nitoke Vipi?,Mabinti wa Kitanga na vinginevyo kupitia albamu yake ya Nitoke Vipi?,alisema mbali na kibao chake hicho Pilato wa Game kuwagusa wengi,anahakika vibao vitakavyokuja baada ya hicho vitakuwa vikali zaidi.
Kibao cha Pilato wa Game kimerekodiwa katika studio za MJ Production chini ya mtayarishaji Marco Chali ambapo video ya kibao hicho imefanyika chini ya kampuni ya Kallaghe's pictures zote za jijini Dar es salaam. Na James Nindi
Monday, June 27, 2011
KIBAO CHA PILATO KIMENITOA-BWANA MISOSI
Monday, June 27, 2011
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment