Wednesday, November 10, 2010

Suma ft steve -Ungejua

Unaweza kuwa unamjua lakini pengine hufahamu mabalaa mengi ya huyu bwana... ana mambo matatu makubwa ambayo pengine wengi wetu twalijua moja tu. Kwanza ni Rapper mkali, pili anauwezo wa ku shoot, ku direct na ku edit music videos, tatu ni brazamen haswaa anapoamua ku upgrade image yake.

Huyu si mwingine bali ni SUMASKILLZ, akiwa msanii wa kwanza kuanguka sign na label mpya ya WA3 Records, chipukizi huyu mkali anaejulikana sana na ngoma yake ya HISIA ZA MTAA (ft STEVE RnB) alipata muda wa kuingia studio za Mlab , DUKETACHEZ akamkabidhi kwa MR. Magician aka WILLIE HD (producer aliyeufanya kazi nzuri sana katika wimbo wa FREE SOUL na NYIMBO zote za grace matata) pamoja na mtu mzima Innocent Mujwahuki a.k.a KANYE (anakumbukwa sana kwa mabalaa yake ya kuhusika partially kwenye productions za nyimbo kama Bado robo saa,wrong SMS, Atatamani na hata nyimbo mpya ya DITO “wapo” hasa kwenye kunyonga milio ya keyboards katika nyimbo hizo).

Baada ya Beat kukaa sawa, mtu mzima SUMA akatupia lines zake pale na jitihada za kumtafua mtu wa kukaa kwenye chorus zikaanza. Inaonekana chemistry ya STEVE RnB haipo tu kwa BABYBOY bali pia hata SUMA nae yupo katika usawa huo..maana mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa mkali huyu wa RnB...baada ya kuita na kutupia zile vocals pale kati hakukuwa hata na mtu mmoja aliebisha studioni. Ngoma ikamaliziwa mixing na mtu mzima DUKETACHEZ mchezo ukaisha.

Hivyo basi kwa mara ya kwanza, Wa3 records ina release single yake ya kwanza kabisa ya label kupitia kwa brazamen SUMASKILLZ aka THE DIRECTOR aka Kichefuchefu. Na hizi hapa ndio ndio details za mzigo mzima:

Artist: SUMASKILLZ feat Steve r’n’b

Song title: Ungejua

Composed By: SUMASKILLZ, Steve r’n’b

Produced by: Willie HD

Mixed By: Willie HD & DUKETACHEZ

Studios: Music Lab

Label: Wa3 records

Zoezi la kupata wasanii wengine katika label limeanza! Utatakiwa kutuma details zako kwa njia ya SMS kwenda namba 15567 pale utakaposikia maelezo kamili kwenye radio na tovuti mbali mbali. Wasanii wanaoanza kutafutwa ni Singers, rappers na producers.

KUTUMA DETAILS ZAKO tuma Wa3 to 15567 na utatozwa Shilingi 1000 kwa huduma hii. na moja kwa moja utapewa maelekezo ya jinsi ya kujiunga. Huduma hii ni kwa wateja wa tiGO, Zain, Vodacom.

Michael Carter Mlingwa

Manager.

0 Comments: