Saturday, November 6, 2010

SAJNA's NEW SONG ft. LINAH-SITAKI KUUMIZWA

"Hello, kwanza nianze kwa kushkuru wote ambao mmeonyesha upendo juu yangu hasa katika kipindi hiki kigumu nilichonacho toka nimepata matatizo mpaka sasa. Naendelea vizuri kiasi, niliruruhiwa kutoka hospitali Ocober 4, ila nikaambiwa natakiwa nipate mapumziko marefu kama miezi m2 au mi 3 bila kufanya kazi ili kukipa nafasi kichwa kiendelee kupona vizuri.


Pia naendelea na madawa na kila baada ya wiki 2 narudi hospitali kuchekiwa navyoendelea. Ila pia wakati natoka hospitali niligundua kuwa jicho moja la kulia halioni ni kama lina ukungu kwa ndani kabisa na mpaka leo hii halioni, dr kaniambia huenda damu ilivyovuja kichwani ilipita pia katika mishipa ya jicho na kuingia jichoni ila niendelee kupumzika huenda likapona lenyewe baada ya muda, hata hapa naandika email kwa shida sana kwa kupitia jicho moja la kushoto.

So muda wote nakuwa nyumbani na ninashinda nimelala au kujiegesha tu kitandani na kusikiliza radio, nimewaeleza yote hayo japo mjue nipo kwenye hali gani.
Pia kuna wimbo mpya wa SAJNA ft. LINAH wa THT . Wimbo huu mpya uanze kuchezwa jumatatu NOVEMBER 8, ila video yake itachelewa kidogo labda mwakani miezi ya mwanzoni kama Mungu atanisaidia nipone haraka, ila mipango ya mwanzo ilikuwa tushoot video yake baada tu ya uchaguzi ila ndio hivyo imenikuta katika hali hii na inatubidi tutoe wimbo mpya.

SONG's DETAILS
Track Name: SITAKI KUUMIZWA
Singer: SAJNA FT. LINAH
lyrics Verse-1, verse-2 and Linah's verse - composed by: KID BWOY
Chorus composed by SAJNA
arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ (Mwanza)

Wimbo unaitwa SITAKI KUUMIZWA, kamshirikisha LINAH wa THT, verse zote hadi za LINAH zimetungwa na SAJNA, ila chorus ndo katunga SAJNA mwenyewe. Ila upande wa IVETA wimbo mzima ailiutunga SAJNA mwenyewe.
Hii sitaki kuumizwa ni mwendelezo wa stori ya IVETA, ukiusikiliza kwa makini utauelewa, ila kwa ufupi ni kwamba yule binti Iveta baada ya kuachwa muda mrefu kule kijijini na mpenzi wake alieenda mjini kutafuta maisha, wazazi wa Iveta walimlazimisha aolewe na jamaa mwingine mwenye pesa alienda mpaka huku kijijini kumchumbia, japo Iveta alikuwa bado anampenda yule jamaa yake wa mwanzo alienda mjini kutafuta ila ikabidi afate maamuzi ya wazazi akaolewa na huyo bwana mpya mwenye pesa na akampeleka mjini kuanza maisha.

Baada ya miezi kadhaa yule mpenzi wa mwanzo wa Iveta akawin maisha kule mjini akaona sasa ni wakati muafaka kumfuata Iveta kijijini ili warudi wote na kuishi mjini. Alipofika kwao Iveta kijijini akatokwa machozi baada ya kuambiwa Iveta ameshaolewa na mwanaume mwingine, ikabidi tu arudi zake mjini.

Jamaa akaamua kuanza maisha mapya na kumsahau Iveta na akaanza mahusiano na msichana mwingine, ila wakaja kukutana na Iveta mjini, (ukiiskiliza verse ya linah ina maneno aliyomwambia huyo X wake kuwa bado anamuhitaji na wazazi ndo walimlazimisha aolewe ila yeye bado anampenda yeye). Pia ukisikiliza chorus na verse za Sajna ndo kuna majibu ambayo jamaa alimpa Iveta baada ya kumwambia bado anamhitaji. Kwa kifupi hiyo ndio stori ya wimbo huu ila ni mwendelezo wa story ya Iveta.

Naombeni sana sana support yenu katika wimbo huu maana mimi bado niko kitandani sina uwezo wowote wa kui push ila nyie ndio tegemeo langu, na asanteni sana kwa kuisukuma IVETA mpaka kufika hapo ilipo.Nisameheeni kwa e-mail ndefu na pia nisameheeni kama nimeiandika vibaya maana sioni vizuri naona kwa jicho moja kwa sasa.
THANX AGAIN

SANDU GEORGE a.k.a KID BWOY
TETEMESHA RECORDS, MWANZA

0 Comments: