Friday, October 1, 2010

NAOMBA MNICHAGUE ILI NILETE MAENDELEO YA KINONDONI-KALAPINA

Kalapina
Mkali wa muziki wa kizazi kipya, Karama Masoud a.k.a Kallapina amesema iwapo atapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia chama cha (CUF)anatarajia kufanya makubwa kwa wakazi wa kata hiyo.

Akichonga na burudanikilasiku jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na yeye kuwa mzaliwa na mkazi wa eneo hilo,anauzoefu wa kutosha kuhusiana na matatizo makubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema kuwa kutokana na yeye kuwa ni mkazi wa eneo hilo,ameweza kuelewa kwa kina matatizo ya wakazi wake na tayari ameanza kufanya mikakati ya kuyapatia ufumbuzi.

"Mimi ni mzalendo na mkazi wa eneo hilo,najua matatizo yote kwamba hatuna soko,miundombinu ni mibovu,hakuna mifeji ya maji taka,haya yote nitayazingatia nikipewa ridhaa ya kuongoza"alisema Kalapina.

Alisema kata yake imekuwa na matatizo mengi zaidi kila kukicha kutokana na viongozi wengi ambao wanapewa nafasi kuongoza kukosa uzalendo.

"Kata yetu inataka kiongozi mzalendo,na mimi nina uzalendo mkubwa kwa kuwa nimezaliwa hapa na kukulia hapa na mpaka sasa naishi katika eneo hili,hivyo matatizo yote nayajua kiundani"alisema.

"Ninaomba wanachama na wananchi wa chama changu kunichagua ili kuhakisha kata yetu inapata kiongozi mzalendo ambaye hakika ataleta maendelea katika kata yetu" alisema.

Source:James Nindi

0 Comments: