Wednesday, September 29, 2010

KWA SASA NAPUMZIKA KUFANYA MUZIKI-SOGG DOGGY

Soggy Doggy
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Anselm Ngaiza a.k.a Soggy Doggy Anter amesema ameamua kuwa kimya kidogo kujihusisha na masuala ya muziki kikamilifu kutokana na hali tete iliyopo katika fani hiyo kwa sasa.

Akichonga na kona hii jijini Dar es Salaam jana msanii huyo alisema pamoja na kuwa na vibao vingi vipya ambavyo amevitunga kwa sasa ameona ni vema kutumia muda wake mwingi katika kazi zake za utangazaji katika kituo cha Redio Uhuru,kilichopo jijini Dar es salaam.

Msanii huyo ambaye alitamba na vibao vyake kadhaa miaka ya nyuma kama vile Kibanda cha Simu, alisema ameamua kukaa kimya kutokana na utata ulipo ndani ya fani ya muziki kwa sasa.
"Biashara ya muziki imekuwa na vizingiti vingi,hivyo nimeamua kutumia muda wangu zaidi kazini kwangu" alisema msanii huyo.

Mbali na hayo,msanii huyu alisema pia amekuwa akitumia nafasi yake ya usanii kuwasaidia wasanii wa kundi lake la Hotpot Familiy kuwapa muongozi wa kimuziki kwa nia ya kusonga mbele. "Hali ya utata wa muziki kwa sisi wakongwe imenifanya kuelekeza nguvu zangu zaidi katika kazi yangu badala na kujihusisha na muziki kwa sasa" alisema msanii huyo.

Msanii huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la Chief Rumanyika alisema pamoja na kuwa kimya siyo kwamba ameacha muziki bali anaendelea kutunga vibao na amekuwa na hazina kubwa ya vibao hivyo katika maktaba yake.


"Sijaacha muziki kabisa,bali nimekaa pembeni kidogo ili kupata muda wa kutosha kufanya kazi zangu na kulisaidia kundi langu la Hotpot Family" alisema msanii huyo.
Soggy Doggy ni mmoja kati ya wasanii walongwe wa muziki huu nchini ambaye alianza kujihusisha na masuala ya muziki tokea akiwa katika masomo yake ya elimu katika shule ya sekondari Jitegemee,Dar es salaam miaka ya tisini.
Source: James Nindi

0 Comments: