
Hapa Lady JayDee akiwapagawisha mashabiki wake

Mpenzi wa Machoz Band akiwa na fulana ya Machozi inayosema "I love Machozi Band"

Keisha naye alikuwepo kumpa Kampani Dada Jay Dee

Mh! sitaki Mie Mwanadada JayDee akimlisha keki Mumewe Gadner

Kaka Issa Michuzi naye akilishwa keki na Jay Dee

Hapa akikata keki ya kutimiza miaka kumi ya kazi yake ya muziki

Mashabiki walimpa sapoti ya kutosha kabisa

Mashabiki walimpa sapoti ya kutosha kabisa


Vijana wa kazi wa Machozi Band wakikamua


Hapa akionyesha bando lililokuwa limeandikwa miaka Kumi ya machozi Band

Mwanadada Lady JayDee majuzi alikuwa anatimiza miaka kumi tangu kuanza kwake muziki maeneo ya Millenium Tower, Kijitonyama na kuzindua albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Combination ambapo katika albamu hiyo kuna wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nilizama. Katika kutimiza miaka kumi ya Machozi Band pia aliimba nyimbo zake za zamani kama vile Mawazo na nyingine nyingi, pia aliungwa mkono na msanii Chege na Keisha katika kutimiza miaka hiyo kumi.
Mdau kutoka Dar. Safina
0 Comments:
Post a Comment