A-Rian
A-Rian ni mtu anayependa kuimba na katika mapumziko yake huwa anapenda kujumuika na washikaji na kusikiliza nyimbo na kucheza na marafiki zake pamoja na familia yake, ni mmoja wa kundi la FAB-K. Alianza kazi hiyo baada ya kuona udhaifu wa muziki uliokuwepo,pia ni mtu anayependa kujifunza kila siku.DJ Eddy
Wasanii wengi wa Uganda hupenda kufanya nae kazi na leo hii ana ujuzi wa kutosha katika kazi hiyo ambaye amefanya soko la muziki nchini Uganda kukua na pia anatengeneza video zilizokuwa na ubora wa kimataifa. Vilevile ni muongozaji mzuri wa video. DJ Eddie anaonekana bora kutokana na kufanya kazi zilizo bora katika soko la muziki.GWM Kiberu
Ebwana wakubwa namtambulisha kwenu Mr. George William Musulira Kiberu (GWM Kiberu). William ndio anayependwa kuitwa pale anapokuwa akiingia ndania ya mitambo ili mashabiki wake wajue kijana wao yuko ndani ya nyumba, ni mtaalamu wa mambo ya habari aliyezaliwa Uganda lakini maisha yake yote yalikuwa UK.Miika Mwamba
Miika Mwamba ni Produza kutoka Finland huyu ni produza aliyewatengenezea nyimbo baadhi ya wanamuziki wa Uganda kama vile Ziggy Dee na wimbo wake wa ‘Eno Mic’, Mad Ice na wimbo ‘Baby Girl’ na wengine wengi na kwa upande wa Tanzania Saida Kaloli na wengine wengi.Ngoni
Ngoni wanaongoza kwa kufanya kazi nzuri, walianza kama kundi na kujipanga na kutengeneza tovuti yao kali iliyotengenezea mipaka mikubwa na sasa wana mategemeo ya kuuendeleza muziki wa Uganda kwa miaka ya baaadae ili uwe wa kimataifa.Kwa sasa wanakuja na programu yao mpya na wanataka baadae Kampala wanataka iwe sio ile waliokuwa wanaijua.Omulangira Suuna
Utakapoulizwa kijana gani anayefanya kazi kwa ajili ya kuwaunganisha wasanii wengi kwa Uganda na nje ya Uganda basi utashindwa kumtaja Omulangira Suuna kwani ni kijana mkali na mwenye ujuzi. Pia ameshafanya kazi na wasanii wengi kama Moses Radio na Weasle ambao walishinda tuzo mwaka jana na wimbo wao ‘Nakudata’ uliotengenezwa katika studio ya Maureen.Peter Kato
Peter Kato a.k.a Produza Peter Kato ni Rais na produza wa Sema Productions Canada. Alianza kazi ya muziki alipokuwa Uganda na katika kipindi hicho alikuwa Uganda akisoma shule ya msingi na alipomaliza aliishi hapo kwa kipindi kirefu na baadae alikuja kuwa rais wa klabu ya drama ambapo ndio iliyomfanya kuwa bora kwa kila alichokuwa akikifanya kuhusiana na muziki kilionekana boraSteve Jean
Ni kijana anayekubarika Uganda na produza mwenye ujuzi kwa kutengeneza nyimbo ambazo kali .Timothy S Kizito
Timothy S. Kizito ni produza mkubwa na Engineer kutoka katika studio ya Bantu Production akiwa na miaka mingi na ujuzi wa miaka 15, kwa upande wa Afrika huwa anapenda kutengeneza nyimbo za Pop, R&B, Hip hop na Raggae.Washington David Ebangit
Huyu ni kijana ambaye yuko kawaida sana kwa muonekano si mwingine bali ni Washington David Ebangit. Baba yake alikuwa ni Dr. Ebangit ambaye ni mchungaji mzuri sana.
Tuesday, January 19, 2010
Maproduza wanaotisha nchini Uganda.
Tuesday, January 19, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment