Jay-ZRihannaJay-ZJay akiwa na Alicia Keys
Wahanga alioathirika na tetemeko la ardhi nchini Haiti wataendelea kusaidiwa na watu mbalimbali wakiwemo wanamuziki kuondokana na umasikini uliowakumba. Kesho Ijumaa tarehe 22 Jay-Z, Alicia Keys, Mary J. Blige, John Legend, Rihanna, Wyclef Jean na wengine wengi watajipanga kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na tetemeko la ardhi nchini humo ambapo ujumbe huo unakwenda kwa jina la “Hope for Haiti Now: A Global Benefit for Earthquake Relief.”
Tamasha hilo linatarajia kufanyika mida ya saa 8PM na kurushwa hewani na vituo mbalimbali kama vile ABC, CBS, NBC, FOX, CNN, The CW, MTV, VH1 na vituo vingine vya burudani. NYC watakaoendesha shughuli hiyo ni kutoka kwa Wyclef Jean, Mary J. Blige huku Jennifer Hudson, Shakira, Bruce Springsteen, na Sting wakiwemo.
Pia katika jiji la Los Angeles Alicia Keys, Justin Timberlake, John Legend, Taylor Swift, Stevie Wonder, Sheryl Crow, Kid Rock na Keith Urban watakuwa ndani ya steji moja.
Jay-Z, U2, Bono na The Edge, Rihanna na Swizz Beatz wataimba wimbo wa pamoja wa taifa la Haiti mjini London.
Thursday, January 21, 2010
Jay-Z, Rihanna, Alicia Keys, U2 na wengine kushiriki kwa pamoja katika kuwasaidia walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Haiti
Thursday, January 21, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment