Wednesday, January 13, 2010

Bobi Wine amnunulia mkewe Range Rover

Nyumbani kwa Bobi Wine
Bobi Wine akiwa na mkewe Barbie
Hii utaweza kuona kama utani ila ni kweli kutokea kwa mpenzi wako au mke kumnunulia zawadi yoyote ila hii ya msanii Bobi Wine wa Uganda hivi majuzi alifanya ‘surprise’ kwa mkewe kwa kumnunulia gari aina ya Range Rover kama zawadi ya krismas na mwaka mpya.

Msanii huyo ambaye ndio msanii mwenye fedha kwa wasanii wa Uganda akifuatiwa na Jose Chameleone alifanya hivyo kama zawadi kwa mkewe Barbie hata hivyo msanii Bebe Cool amekasirishwa kwa kitendo cha yeye kumnunulia gari hiyo mkwewe.

Gari hiyo aliyonunua Bobi Wine ni gari anayotembelea Bebe Cool ambayo yeye ndio anaona ni gari ya thamani kwa sasa anaona kama ni dharau kwa Bobi Wine kumnunulia mkewe Range Rover na yeye anataka kumnunulia mkewe Zuena ili kujibu mapigo aliyofanya Bobi Wine.

Japo Bebe Cool na Bobi Wine ni rafiki katika ushindani katika muziki ila kwa hili itambidi Bebe Cool kufanya lile linalowezekana kumshinda Bobi Wine alichokifanya kwa mkewe Barbie.

0 Comments: