Wednesday, December 30, 2009

Kleptomaniax yakamilisha albam ya tatu


Kundi la Kleptomaniax la Kenya liliotamba kipindi cha nyuma na kupotea kabisa katika ramani ya muziki sasa linarudi tena likiwa na Roba, Nyash na Collo.

Akichonga na kona hii mmoja wa wasanii wa kundi hilo Collo amesema kuwa kundi hilo limeshakamilisha albamu yao ya tatu ambayo mpaka sasa wameshatoa albamu ya pili.

Katika kazi hizo walipata kutamba na nyimbo zao kali zilizoshika kwa Afrika Mashariki kama vile Haree, Tuendelee na wamefanya na wakali wa kutengeneza muziki wa Ogopa Djs.

Msanii mwenzao Nyanshinky ambaye alitamba katika wimbo wa amani wa Bad Boy ambaye anapiga buku kiwanja Marekanina kuwaacha wenzake Roba na Collo wakipeperusha bendera la kundi lao la Klepto ambapo Nyashinsky akimaliza masomo yake na kuja kujiunga na kundi lake hilo hivi karibuni.

Kundi hilo ambalo lilifanya vizuri katika anga ya muziki kwa Afrika mashariki na kuweza kushiriki katika tuzo mablimbali za muziki kama vile tuzo za Chaguo la Teeniez award, Kisima Award na MTV Europe award na kujinyakulia tuzo hizo na nyimbo zao za Haree na Tuendelee.

Wasanii hao kwa sasa wamejikita katika muziki kwa kasi ya juu baada ya kupotea kwa muda mrefu katika anga ya muziki hadi kuonekana kama wameshindwa muziki,ambapo mashabiki walijua wameshindwa baada ya kutoa wimbo wao wa Tuendelee.

Alipoulizwa Collo juu ya bifu na makundi ya kenya juu ya wimbo wao wa Tuendelee ulikuwa na njia ya kuwatukana wanamuziki fulani wa Kenya alisema sio kweli kwani wimbo huo waliotoa baada ya kuona baadhi wa watu wanasema walikuwa wanabahatisha muziki waliokuwa wakiufanya.

0 Comments: