Saturday, July 1, 2017

Wasiozingatia usafi wamkera Lulu

BINTI anayetesa kwenye tasnia ya filamu nchini  Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameoneshwa kukasirishwa na vitendo vya uchafu kwa baadhi ya waumini makanisani.
Akizungumza hivi karibuni Lulu anasema waumini wawapo kanisani na hata nje wanatakiwa kuzingatia usafi wa mwili na roho kwani kuna muda huwa wanasalimiana wanapokuwa kwenye ibada, hivyo kama hawatazingatia usafi huenda ikaleta taabu katika kukamilisha misa au ibada.
“Mnaowekaga vidole puani kanisani, hamjui kama kuna ule muda wa kupeana mikono au mnatakaga kugundua nini? Tuwe wasafi wa roho na mwili,”ameandika Lulu kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo mrembo huyo ameongeza kuna siku moja alimuona muumini mmoja akishika pua na leo ameamua kumpa makavu kwa kumuelimisha.
“Kuna muumini mmoja alifanya hivyo pembeni yangu leo sijampa mkono bali nimempa ukweli,”anasema Lulu.

0 Comments: