Monday, September 19, 2011

EXCLUSIVE INTERVIEW AVRIL FROM KENYA


Born Judith Nyambura Mwangi in 30th April 1986 in Nakuru, Kenya. Studied in Kenya and Uganda for elementary school, O and A levels and holds a Design degree from the University of Nairobi. Is currently signed to the Ogopa Deejays label and released a debut single entitled 'Mama'. Has worked with a number of artists in Kenya as well as East Africa such as A.Y from Tanzania and LAM from Sudan.

Haya sasa kwa hapo tu utakuwa umemjua vizuri mwanadada huyu aliyemghalisha Ay katika Remix ya Leo, si mwingine bali ni Judith Nyambura Mwangi "Avril". Na leo tuna EXCLUSIVE INTERVIEW ya maswali mawili matatu juu ya kazi aliyofanya na wasanii kwa Afrika Mashariki.

Mpaka sasa umeshafanya kazi na wasanii wangapi ili watu mbalimbali wajue , " Mimi ni msanii mpya kwenye industry ya Kenya na Afrika Mashariki so, nina wimbo nyimbo yangu ya 'Mama' na sasa tuna nyimbo inayofanya vizuri katika soko ya Chokoza tuliyofanya na Marya na katika albamu yangu ninayoiandaa nimeshirikiana na baadhi ya wasanii kama Jaguar (Kenya), Kenzo (Kenya), Trapee (Kenya), Moustapha toka kundi cha Deux Vultures (Kenya), Collo toka kundi cha Kleptomaniacs (Kenya), King Georges (Kenya), A.Y (Tanzania), LAM (Sudan).

Hivi unajua ni nani aliyemshawishi mpaka kufanya muziki huyu si mwingine bali ni produza wake Lucas Bikedo ambaye amewafanikisha wasanii mablimbali kuingia katika industry ya muziki na kazi kibao za 'background vocals'.

Hivi ilikuwaje mpaka ukafanya kazi na Mzeyaa AY kwenye nyimbo yake ya Leo Remix , " Nilijisikia nimebarikiwa sana kufanya kazi na A.Y kwani ni msanii mkubwa sana Afrika Mashariki na alinipa moyo kuhusiana na soko la muziki kwa East Afrika kama rafiki na ndugu kwahivyo akanifunza mengi sana.

Unajua Avril huwa anapenda sana kufanya nyimbo za aina zipi,” Ninapenda kufanya muziki aina ya Contemporary Urban kwani aunibani kufanya lolote nitakachohisi kinanipendeza kwa kuandika muziki".

Avril has now come out with a strongly worded denial?

"Oh my lord. They have been working hard to bring me down but I don’t care how far they go with it. It was a set up,”. Even though the Mama and Chokoza singer does not admit knowledge of ever having taken such photos or having a romantic affair with another female, her manager points to “a fellow player in the showbiz industry”. “You can read malice in the whole thing. These are showbiz wars made to discredit Avril as a popular figure and Ogopa as a recording stable. Investigations are underway and we are closing in on the suspects. But we won’t divulge any further information for now,” said Emmanuel Banda, the Ogopa artistes’ manager."

Hivi Avril kitu kinachomkera kabisa katika maisha yako ni nini?. " Kinachonikera sana ni kupenda kuwapa nafasi wasanii toka ng'ambo na kusahau wasanii wetu wa hapa Afrika. Pia sio vibaya kuwa na 'music radio stations' kwa runinga zikionyesha muziki wa Afrika pekee na kuacha kupiga muziki toka ng’ambo, lakini sio vibaya local content ikiwa chini ya asilimia hamsini.

Pia nilimuuliza katika maisha kila mtu huwa na lengo analokuwa nalo ila kwa Avril alisema kuwa ni kuwa mwanamuziki atakaetambulika Afrika na dunia kwa ujumla na aweze kuwa 'role model' kwa wasichana kama yeye tofauti na wanamuziki wengine.

Avril anavipaji kibao moja katika vipaji vyake nje ya muziki anaufanya ni mwanachuo wa Design katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Na pia anatarajia akimaliza chuo mwaka ujao na atatumia ustadi wake wa design kwa kuboresha muziki wake na kuwa na brand yake kama Avril.


For more detail visit:

0 Comments: