Wednesday, November 23, 2016

COYO AJA NA UJIO MPYA ‘NJOO BAADAE’



Inline image 1
 
Baada ya kuachia video/wimbo wake wa kwanza ‘NOMA’ miezi michache iliyopita, msanii Coyo ambaye ni mwenyeji wa jiji la miamba, Mwanza anatambulisha kazi yake mpya NJOO BAADAE, ikiwa ni ya pili kuachiwa akiwa chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment.

Akizungumzia wimbo wake mpya, Coyo anasema, “NJOO BAADAE ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila siku ya vijana”.


“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe zako ambazo haziendani na stori  zake, hivyo unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae.” Ameongeza.

NJOO BAADAE imeandikwa na Coyo ambaye pia amefanya viitikio vya kuimba, na muziki wake umeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi wa Tetemesha Ent.

                                                               
Wimbo wa NJOO BAADAE pamoja na Instrumental vimeambatanishwa hapa, share na wengine kadri uwezavyo.


Tazama mashahiri ya NJOO BADAAE hapa: https://youtu.be/llLrVJvPeok               

Tazama video yake iliyopita ‘NOMA’ hapa: https://youtu.be/VEPUTJL_Tj8


Editor’s Notes:
·         Kwa sasa Coyo amehamishia makazi yake jijini Dar es salaam ili kurahisisha shughuli zake za kimuziki
Tafsiri ya mistari ya kisukuma kwenye verse ya kwanza na ya pili.
·         Wabeja  (Asante)
·         Lekaga tuja( acha dharau)
·         Nale na shida shane  (nipo na shida zangu)
·         We nitakupeja  (we nitakukimbiza/kufukuza)

KWA MAHOJIANO:

MITANDAO YA KIJAMII:
www.instagram/ coyotz1

MANAGEMENT CONTACT:

0 Comments: